BEKI mpya wa Manchester United, Marcos Rojo hatacheza leo dhidi ya MK Dons kutokana na kwamba bado hajapata kigali cha kufanyia kazi nchini Uingereza.
Louis van Gaal alitarajia kumtumia Rojo katika mchezo waliomaliza kwa safe ya kufungana bao 1-1 na Sunderland Jumapili, lakini sasa atamsikilizia katika mchezo wa genii dhidi ya Burnley Jumamosi.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 24, amekamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 16 Man United wiki iliyopita, lakini atalazimika kusubiri hadi patine kigali cha kufanyia kazi.
Subiri kijana: Marcos Rojo (kulia) hatakuwepo katika mchezo dhidi ya MK Dons kwa sababu ya kibali cha kufanyia kazi Uingereza
Rojo anaingia kwenye orodha ndefu ya wachezaji wanaokosekana uwanjani kwa sasa United, wengine wakiwa ni Luke Shaw, Michael Carrick, Marouane Fellaini, Jesse Lingard, Rafael da Silva na Ander Herrera ambao wote ni majeruhi.
Van Gaal anatarajiwa kuendelea kuwapa nafasi wachezaji chipukizi usiku wa Jumanne kama Michael Keane na Tyler Blackett katika kikosi cha kwanza kwenye mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment