KIUNGO aliyeshindwa kung'ara Manchester United, Shinji Kagawa amekamilisha uhamisho wa kurejea Borussia Dortmund kwa dau la Pauni Milioni 6.3, miaka miwili tu tangu aondoke klabu hiyo ya Ujerumani.
Kagawa atasaini Mkataba wa miaka minne na Dortmund, ambayo ilimuuza Mjapani huyo United mwaka 2012 kwa Pauni Milioni 12.
Lakini kuumia umia mara kwa mara kulimkwamisha mchezaji huyo kung'ara na baada ya kufeli mbele ya kocha David Moyes msimu uliopita, kocha Louis van Gaal amemtema.
0 comments:
Post a Comment