// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); GIROUD AINUSURU ARSENAL KULALA KWA EVERTON, SARE 2-2 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE GIROUD AINUSURU ARSENAL KULALA KWA EVERTON, SARE 2-2 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, August 23, 2014

    GIROUD AINUSURU ARSENAL KULALA KWA EVERTON, SARE 2-2

    BAO la dakika ya mwisho la Olivier Giroud limeipa sare ya ugenini Arsenal katika mchezo wake wa pili wa Ligi Kuu ya England baada ya kufungana mabao 2-2 na Everton
    Kocha Arsene Wenger alimtumia Alexis Sanchez kama mshambuliaji pekee kabla ya kumpumzisha baada ya dakika 45 za kwanza, wakati Mesut Ozil alimchezesha wingi ya kushoto na alichangia bao la kwanza.
    Mwokozi; Olivier Giroud akishangilia baada ya kuifungia bao la kusawazisha Arsenal dakika ya 90

    Seamus Coleman alitangulia kuifungia Everton kwa kichwa dakika ya 19, kabla ya Steven Naismith kufunga la pili dakika ya 45 licha ya kwamba alikuwa ameotea.
    Aaron Ramsey aliifungia bao la kwanza Arsenal dakika ya 83, kabla ya Giroud kusawazisha dakika ya 90. 
    Kikosi cha Everton kilikuwa; Howard, Coleman, Jagielka, Distin, Baines, McCarthy, Barry, Mirallas/Atsu dk85,Naismith, Pienaar/Osman dk10 na Lukaku/McGeady dk76.
    Arsenal; Szczesny, Debuchy, Chambers, Mertesacker, Monreal, Flamini, Oxlade-Chamberlain/Campbell dk74, Ramsey, Wilshere/Cazorla dk74, Ozil na Sanchez/Giroud dk46.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GIROUD AINUSURU ARSENAL KULALA KWA EVERTON, SARE 2-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top