KIUNGO Angel di Maria amewasili viwanja vya mazoezi vya Manchester United, Carrington kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wa Pauni 60 kutoka Real Madrid ya Hispania.
Nyota huyo wa Argentina aliyeng'ara kwenye Kombe a Dunia amewasili England huku viongozi wa Old Trafford wakiendelea na mazungumzo na Real Madrid juu ya kukamilisha uhamisho wa dau la rekodi Uingereza.
Di Maria, mwenye umri wa miaka 26, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake usiku huu ambao utamfanya alipwe Pauni 200,000 kwa wiki kwa zaidi ya miaka mitano, mshahara ambao pia utamfanya awe mchezaji wa pili kulipwa zaidi katika klabu hiyo baada ya Nahodha, Wayne Rooney.
Di Maria anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake usiku huu
Uhamisho wote utaigharimu United zaidi ya Pauni Milioni 90 na mchezaji huyo ataingia moja kwa moja katika kikosi kilichojeruhiwa cha Louis van Gaal kwa ajili ya mchezo dhidi ya timu iliyopanda Ligi Kuu, Burnley.
0 comments:
Post a Comment