// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); STARS WAWASILI SALAMA JOHANNESBURG, BALOZI AWATEMBELEA VIJANA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE STARS WAWASILI SALAMA JOHANNESBURG, BALOZI AWATEMBELEA VIJANA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Thursday, July 31, 2014

        STARS WAWASILI SALAMA JOHANNESBURG, BALOZI AWATEMBELEA VIJANA

        Na Boniface Wambura, JOHANNESBURG
        KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kimewasili salama jana (Julai 30 mwaka huu) hapa Johannesburg kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kwenda Maputo, Msumbiji kwa ajili ya mechi dhidi ya Mambas itakayochezwa Jumapili.
        Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefanya mazoezi mara mbili leo- asubuhi na jioni kwenye uwanja wa Bedfordview Country Club. Mazoezi ya mwisho yatafanyika kesho asubuhi (Agosti 1 mwaka huu) kabla ya baadaye jioni kuanza safari ya Maputo.
        Wachezaji wa Taifa Stars wakati wanaondoka Dar es Salaam jana

        Wakati huo huo, Balozi wa Tanzania hapa Afrika Kusini, Razia Msuya baadaye leo jioni atazitembelea timu zote mbili za Tanzania zilizopo hapa Johannesburg kusalimia wachezaji.
        Serengeti Boys yenyewe ipo hapa tangu Julai 27 kwa ajili ya mechi dhidi ya Afrika Kusini itakayochezwa Jumamosi (Agosti 2 mwaka huu).
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: STARS WAWASILI SALAMA JOHANNESBURG, BALOZI AWATEMBELEA VIJANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry