Na Mahmoud Zubeiry, BETHLEHEM
ALIYEKUWA kocha wa Yanga SC, Mbelgiji Tom Sainfiet amesema kwamba aliondoka kwenye klabu hiyo akiwa bado anaipenda, kwa sababu Mwenyekiti, Yussuf Manji aliamua.
“Baada ya kufanya nao kazi vizuri katika Kombe la Kagame na tukawa mabingwa, nilipanga kujitolea zaidi kuifikisha mbali zaidi ile klabu, lakini kusema ukweli kulileta mtafaruku, tukatengana,”alisema Sainfiet akizungumza na BIN ZUBEIRY jana mjini hapa.
“Manji ndiye kila kitu pale Yanga, anaweza kuamua anachotaka na mtu yeyote asimpinge, imebaki historia, ila sina ubaya na Yanga, bado nina mawasiliano na baadhi ya wachezaji na hata baadhi ya viongozi. Abdallah (Bin Kleb) tunaendelea kuwasiliana, tuna maelewano
mazuri,”amesema.
Kocha huyo mpya wa Free State Stars ya Ligi Kuu ya hapa, aliipa ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kagame Yanga SC mwaka 2012, lakini akafukuzwa baada ya siku 80 kwa kusema ukweli.
Alilalamikia hali ya wachezaji kulazwa watatu katika kitanda kimoja kwenye hoteli ilipokwenda kwenye mechi za Ligi Kuu mikoa ya Kagera na Mbeya na aliporudi Dar es Salaam akaitwa na Manji na kuvunjiwa Mkataba.
Baadaye Yanga iliwafukuza pia aliyekuwa Katibu Mkuu, Selestine Mwesigwa na Ofisa Habari, Louis Sendeu walioongozana na timu Bukoba wakidaiwa kuwa chanzo cha timu kulala ‘mzungu wa nne’.
Alipoulizwa kama anaweza kurudi Yanga SC siku moja, Saintfiet alisema; “Sina tatizo na Yanga, niliondoka pale bado naipenda, tatizo alikuwa Manji,”alisema.
Sainfiet aliyerithi mikoba ya Mmalawi Kinnah Phiri Free State mwishoni mwa mwezi uliopita, amesema alikaribia kujiunga na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Machi mwaka huu, lakini Yanga ikamnyima nafasi hiyo.
“Malinzi (Jamal), Rais wa TFF aliniambia rekodi yangu ni nzuri na wasifu wangu ni mzuri, lakini wanaogopa kunipa Mkataba kwa sababu niliwahi kufanya kazi Yanga, alisema nikiwa kocha wa timu ya taifa nitawagawa mashabiki. Nikakubali, nilienda Malawi na sasa nipo hapa,”amesema.
Mholanzi Maart Nooij alirithi mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen Taifa Stars Aprili mwaka huu.

Saintfiet akiwa na Mtendaji Mkuu wa BIN ZUBEIRY Blog, Mahmoud Zubeiry leo |
Kocha huyo mpya wa Free State Stars ya Ligi Kuu ya hapa, aliipa ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kagame Yanga SC mwaka 2012, lakini akafukuzwa baada ya siku 80 kwa kusema ukweli.
Alilalamikia hali ya wachezaji kulazwa watatu katika kitanda kimoja kwenye hoteli ilipokwenda kwenye mechi za Ligi Kuu mikoa ya Kagera na Mbeya na aliporudi Dar es Salaam akaitwa na Manji na kuvunjiwa Mkataba.
Baadaye Yanga iliwafukuza pia aliyekuwa Katibu Mkuu, Selestine Mwesigwa na Ofisa Habari, Louis Sendeu walioongozana na timu Bukoba wakidaiwa kuwa chanzo cha timu kulala ‘mzungu wa nne’.
Saintfiet akiwa na Mrisho Ngassa leo |
Alipoulizwa kama anaweza kurudi Yanga SC siku moja, Saintfiet alisema; “Sina tatizo na Yanga, niliondoka pale bado naipenda, tatizo alikuwa Manji,”alisema.
Sainfiet aliyerithi mikoba ya Mmalawi Kinnah Phiri Free State mwishoni mwa mwezi uliopita, amesema alikaribia kujiunga na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Machi mwaka huu, lakini Yanga ikamnyima nafasi hiyo.
“Malinzi (Jamal), Rais wa TFF aliniambia rekodi yangu ni nzuri na wasifu wangu ni mzuri, lakini wanaogopa kunipa Mkataba kwa sababu niliwahi kufanya kazi Yanga, alisema nikiwa kocha wa timu ya taifa nitawagawa mashabiki. Nikakubali, nilienda Malawi na sasa nipo hapa,”amesema.
Mholanzi Maart Nooij alirithi mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen Taifa Stars Aprili mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment