KLABU ya Real Madrid imekubali kumsajili mfungaji bora wa Kombe la Dunia, James Rodriguez kutoka Monaco kwa mkataba wa miaka sita.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Colombia amekubali kusaini mkataba wa miaka sita Madrid baada ya kufuzu vipimo vya afya leo. Atatambulishwa jioni ya leo.
Hakuna ofa iliyothibitishwa na klabu hiyo kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, lakini taarifa zinasema Madrid imelipa kiasi cha Pauni Milioni 60, ambazo zinamfanya Rodriguez awe mchezaji mamba tatu ghali duniani kihistoria baada ya Gareth Bale, Cristiano Ronaldo na Luis Suarez.
0 comments:
Post a Comment