KLABU ya Arsenal imekamilisha usajili wa kipa wa Nice, David Ospina kwa dau la Pauni Milioni 3.2, kwa mujibu wa kocha wa klabu hiyo ya Ufaransa, Claude Puel.
Ospina aliivutia The Gunners kufuatia kuranya vizuri akiidakia Colombia katika Kombe la Dunia hadi kuifikisha Robo Fainali, ambako walitolewa na wenyeji, Brazil.
Mlinda mango huyo mwenye umri wa miaka 25 anajiunga na timu hiyo ya Kaskaizni mwa London kwa mkataba wa miaka minne. Puel amezungumzia habari za kuondoka kwa Ospina alipohojiwa na Sky Sports na kusema: "Imethibitishwa, ndiyo. Akiwa na umri wa miaka 25 ni muhimu kwake kupata uzoefu wa mashindano mengine, hivyo ni uhamisho mzuri wake,".
Uwezo utamuweka mtu langoni: David Ospina (kushoto) atagombea mamba na kipa wa sasa wa kwanza wa Arsenal, Wojciech Szczesny
Inafahamika kwa sasa kipa huyo anakwenda kuchukua nafasi ya Lukasz Fabianski, ambaye amejiunga na Swansea, kwenda kuwa wa pili nyuma ya kipa namba moja wa sasa wa klabu hiyo, Wojciech Szczesny.
Pamoja na hayo, kocha Arsene Wenger amesema uwezo ndio utakaomfanya mmoja wao awe kipa mamba moja wa klabu, huku Ospina akionekana kabisa kuitaka kuwa chaguo la kwanza.
"Unajua mwanzoni Szczensy atakuwa mamba moja, kisha tena uwezo wa mtu ndiyo utaamua, ikiwa Ospina ataonyesha ni bora, atacheza,"aliiambia ESPN.
0 comments:
Post a Comment