MSHAMBULIAJI Alvaro Negredo atakuwa nje ya Uwanja kwa miezi mitatu baada ya kuumia kikanyagio cha mguu wa kuli katika mchezo wa kirafiki baina ya Manchester City na Hearts.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amethibitisha taarifa za kuumia kwake kwa kuposti picha ya mguu wake ukiwa umefungwa kizuio, lakini amesema atarajea akiwa ana nguvu kuliko alivyowahi kuwa daima.
"Nataka ujue kwamba itakuwa ngumu kwa miezi michache ijayo," ameposti. "Nimevunjika mguu na nitakuwa nje kwa miezi michache. Nitarudi mwenye nguvu kuliko daima,".
Nje: Mshambuliaji wa Manchester City, Alvaro Negredo atakuwa nje kwa miezi mitatu baada ya kikanyagio kuvunjika mguu
Mguu wa Negredo alivyouposti kuthibitisha kuumia kwake
Pamoja na hayo, mchezaji huyo anayekwenda kwa jina la utani 'The Beast' amesema anafurahia City na hana mpango wa kuwahama mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England.
0 comments:
Post a Comment