// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MOURINHO: NIMEFUNGA USAJILI CHELSEA, COSTA, FABREGAS NA LUIS WANATOSHA, SASA NATAKA KUPANDISHA WATOTO WA AKADEMI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MOURINHO: NIMEFUNGA USAJILI CHELSEA, COSTA, FABREGAS NA LUIS WANATOSHA, SASA NATAKA KUPANDISHA WATOTO WA AKADEMI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, July 25, 2014

    MOURINHO: NIMEFUNGA USAJILI CHELSEA, COSTA, FABREGAS NA LUIS WANATOSHA, SASA NATAKA KUPANDISHA WATOTO WA AKADEMI

    KOCHA Jose Mourinho amesema Chelsea imemaliza usajili wa kununua wachezaji na sasa anataka kupandisha chipukizi kutoka timu za vijana.
    The Blues imemwaga fedha kuwasajili Cesc Fabregas, Diego Costa na Filipe Luis, na kwa muda mrefu haijapndisha mchezaji kutoka kwenye akademi yake tangu Nahodha wake wa muda mrefu, John Terry.
    Lakini kocha Mourinho amesema kwamba wachezaji hao wapya wanatosha kuongeza nguvu katika kikosi kilichofika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.

    Anawapa nafasi vijana: Jose Mourinho atapandisha vijana wa U-21 kikosi cha kwanza Chelsea

    CHIPUKIZI WATANO WA KUMULIKWA CHELSEA

    1. Jeremie Boga
    2. Izzy Brown
    3. Patrick Bamford
    4. Marco Van Ginkel
    5. Kurt Zouma
    Alipoulizwa kama kikosi chake kitakuwa na sura mpya zaidi Stamford Bridge, Mourinho alisema: "Sifikirii hivyo". 
    "Soko lipo wazi, lakini tuna furaha na tulichonacho. Tunafikiri kwamba, kikosi chetu ndicho tulichokitaka.
    "Hatutaki kikosi cha wakongwe watupu, pia tunataka kuingiza katika kikosi cha kwanza wachezaji watatu, wanne au watano wa U-21na kuendeleza wachezaji, hivyo tuna furaha na uwiano uliopo ndani ya kikosi,".
    Chipukizi wa Chelsea wamekuwa kivutio katika mechi za kujiandaa na msimu, Jeremie Boga akiinusuru The Blues kulala katika mchezo wa kwanza wa ziara ya kujiandaa na msimu nchini Austria dhidi ya RZ Pellets akifunga bao lililofanya sare, wakati Patrick Bamford na Izzy Brown wote walifunga dhidi ya Wycombe.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MOURINHO: NIMEFUNGA USAJILI CHELSEA, COSTA, FABREGAS NA LUIS WANATOSHA, SASA NATAKA KUPANDISHA WATOTO WA AKADEMI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top