KIUNGO Frank Lampard amekamilisha uhamisho wake klabu ya New York City FC ya Ligi Kuu ya Marekani, maarufu MLS na kutambulishwa leo.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 36 ameondoka Chelsea mwishoni mwa msimu baada ya kuichezea kwa misimu 13 akiweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa kihistoria wa klabu hiyo kwa mabao yake 211.
Kiungo huyo anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa New York City FC na wa pili mwenye nina kubwa, baada ya David Villa kutoka Atletico Madrid.
0 comments:
Post a Comment