VIKOSI viwili vilivyoshinda mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa awamu tofauti jana viliungana kuichezea Barcelona katika mechi dhidi ya FC Porto, kumuaga kiungo wa zamani wa kimataifa wa Ureno, Deco.
Mchezo huo uliowahusisha wachezaji nyota kama Lionel Messi, Eidur Gudjohnsen, Benni McCarthy na Paulo Ferreira, ulimalizika kwa sare ya 4-4, huku Samuel Eto'o akifunga mabao mawili na Deco aliyechezea nusu moja kila timu, akiifungia bao moja kila timu, likiwemo la mwisho la Porto lililoamua matokeo.
Mabao ya Porto yalifungwa na Derlei dakika ya tatu, McCarthy dakika ya 15, Jankauskas dakika ya 62 na Deco dakika ya 89, wakati ya Barca yalifungwa na Eto'o dakika za 54 na 68, Deco 57 na Messi 81.
Kikosi cha Porto kilikuwa: Baia, Ferreira, Costa, Emanuel, Valente, Costinha, Maniche, Mendes, Deco/Jankauskas dk46, Derlei na McCarthy.
Barcelona: Jorquera, Oleguer, Belletti, Gerard, Sylvinho, Davids, Van Bommel, Van Bronckhorst, Giuly/Deco dk46, Ezquerro/Eto'0 dk46 na Gudjohnsen/Messi dk46.
Messi na Deco wakimpongeza Eto'o baada ya kufunga
Magwiji: Samuel Eto'o na Deco wakisalimiana Uwanja wa Estadio de Dragao mjini Porto kabla ya mchezo
Messi akiwatoka mabeki wa Poro
Benni McCarthy akipambana katikati ya Sylvinho na Oleguer
0 comments:
Post a Comment