KOCHA mpya wa New AC Milan, Pippo Inzaghi amesema a tampa nafasi nyingine mshambuliaji Mario Balotelli kudhihirisha umuhimu wake katika timu- maana yake mpango wa kuhamia Arsenal umekufa kifo cha kawaida.
Inzaghi aliichezea mechi zaidi ya 200 The Rossoneri, akishinda nato mataji mawili ya livi na mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na baada ya uongozi wa klabu kumchoka Balotelli kiasi cha kutaka kumuuza, mkongwe huyo ameweka wazi anampa nafasi tena.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 40 amesemad: "Balotelli ni mchezaji muhimu sana na mali ya Milan. Nitamchukulia yeye kama ninavyowachukulia wachezaji wengine,"amesema.
"Nitasahau kila kitu nilichosikia kuhusu yeye kiwi kibaya au kizuri, kwa sababu nataka kuwajua watu ili kupata undani wao,".amesema kocha huyo ambaye yupo Marekani na kikosi chake kwa maandalizi ya msimu mpya.
Inzaghi amechukua nafasi ya mchezaji menzake wa zamani, Clarence Seedorf kuikochi Milan lakini tayari ameweka wazi namna ambavyo Balotelli anafaa katika mipango yake.
Inzaghi akiwa na shabiki mjini New York
Balotelli akiwa na Keisuke Honda Sulley Muntari
0 comments:
Post a Comment