MABAO ya Diego Costa na Kurt Zouma yameipa Chelsea ushindi wa 2-1 dhidi ya Olimpija Ljubljana jioni hii nchini Slovenia katika mchezo ambao Didier Drgoba aliyerejeshwa tena Stamford Bridge alikuwa benchi.
Kikosi cha Jose Mourinho kililazimika kupambana na kutoka nyuma kwa bao 1-0 hadi mapunziko baada ya Nik Kapun kuifungia timu hiyo ya Slovenia bao la kuongoza. Lakini mabao ya kipindi cha pili ya Costa na Zouma yaliipa The Blues ushindi ikitoka nyuma.
Branislav Ivanovic alifikiri amefunga bao la tatu, baada ya awali kukubaliwa, lakini ghafla refa akabadilisha mawazo yake na kukataa bao hilo.
Kikois cha Chelsea kilikuwa: Delac/Cech dk46, Azpilicueta/Ivanovic dk46, Cahill/Terry dk46, Zouma, Luis/Ake dk46, Matic,Solanke, Fabregas/Romeu dk69, Salah/Chalobah dk72, Boga/Van Ginkel dk46, Brown/Torres dk46 na Costa/Bamford dk72.
Mtu hatari: Mshambuliaji wa zamani wa Atletico Madrid, Costa akikimbia baada ya kufunga bao lake la kwanza akiwa na jezi ya bluu ya Chelsea
Diego Costa akijiandaa kufunga
Costa akipambana na Antonio Mlinar Delamea
Orders: Manager Jose Mourinho shouts instructions from the half way line as his team take on Olimpija
Kurt Zouma (wa pili kushoto) akishangilia bao lake na Mohamed Salah
Kiungo wa zamani wa Arsenal na Barcelona, Fabregas alikuwa kivutioa leo
Mchezaji mpya, Filipe Luis (kulia) akipambana na Nik Omladic (kushoto)
0 comments:
Post a Comment