BEKI Mats Hummels yuko mbioni kujiunga na Manchester United wiki hii akitokea Borussia Dortmund kwa dau la Pauni Milioni 16, kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania.
Klabu hizo mbili bado hazijafanya mazungumzo kwa ajili ya uhamisho huo, lakini timu ya Old Trafford inajiamini mno inaweza kumpata beki huyo hodari.
Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 25 aling'ara kwenye Kombe la Dunia akiwa na Ujerumani iliyoibuka bingwa nchini Brazil, kiasi cha kumvutia hadi kocha mpya wa United, Louis van Gaal.
0 comments:
Post a Comment