Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM AZAM FC imetwaa ubingwa wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kwa nchi za Maziwa Makuu, maarufu kama Rollingston baada ya kuichapa timu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ya Mgulani Twalipo bao 2-0 katika fainali jioni hii Uwanja wa karume, Dar es Salaam. Jamil Mchaulu ‘Balotelli’ aliyefunga bao la kwanza dakika ya tatu, baada ya kuwatoka vizuri beki wa kulia wa Twalipo, Ally Mbonde na beki wa kati Ally Athumani kisha kumtungua kipa wao, Kulwa Baumba.
Jamil Balotelli kushoto akimiliki mpira pembeni ya mabeki wa Twalipo leo Uwanja wa Karume
Beki wa Twalipo akimpunguza kasi winga wa Azam FC, Farid Mussa
Twalipo ilipoteza mwelekeo mapema tu baada ya bao hilo, na wachezaji wake kuanza kucheza rafu nyingi, badala ya kutengeneza mipangop ya kusawazisha bao. Azam walitumia mwanya huo kucheza mpira wa kuachiana pasi za haraka uwanjani kuwakwepa ‘wapiga kiatu’ wa jeshini na kufanikiwa kumaliza dakika 45 za kwanza wakiwa wanaongoza 1-0.
Kikosi cha Azam FC leo
Jamil Balotelli akimtoka mtu
Wachezaji wa Champion na Bom Bom wakionyeshana kazi
Kipindi cha pili, mchezo ulizidi kunoga, Twalipo wakisaka bao la kusawazisha na Azam wakitafuta mabao zaidi- hali iliyosababisha mashambulizi ya pande zote mbili. Alikuwa ni Adam Omar Soba aliyeihakikishia Kombe la kwanza la Rollingston Azam FC baada ya kufunga bao la pili dakika ya 88. Katika mchezo wa kwanza wa kuwsaka mshindi wa tatu, Champion ya Kawe ilitwaa ubingwa wa U17 kwa kuifunga 1-0 Bom Bom ya Ilala kwenye Uwanja huo huo, Karume.
Samuel Eto’o eyes CAF Exco seat
-
Cameroonian Football Football (FECAFOOT) president Samuel Eto’o is keen to
become a member of the Confederation of African Football (CAF)’s executive
com...
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment