KLABU ya Arsenal imekubali kutoa Pauni Milioni 3.2 kwa ajili ya kumnunua kipa wa Nice, David Ospina.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 aling'ara na Colombia wakati wa Kombe la Dunia na anatarajiwa kumpa changamoto Wojciech Szczesny. Ospina amekataa ofa ya Valencia.
Ospina alikuwa mmoja wa makipa waliokuwa kivutio kikubwa katika Kombe la Dunia, hakiiwezesha Colombia kufika Robo Fainali, ambako ilitolewa na wenyeji Brazil.
Wakati huo huo; Arsenal, inamtaka pia kiungo wa Sporting Lisbon mwenye thamani ya Pauni Milioni 35, William Carvalho.
Tayari Arsenal imemsajili mshambuliaji nyota wa Chile,A lexis Sanchez kutoka Barcelona
0 comments:
Post a Comment