KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho anafikiri no vyema Chama cha Soka England (FA) kikatumia fedha inazokuanya kwa kuwatoza faini wachezaji, klabu na makocha nchini humo kwa kuchangia miradi ya hisani.
Kuliko kwenda kuangalia Kombe la Dunia nchini, Mourinho amezuru nchini Ivory Coast kuwatembelea watoto wenye njaa na waathirika wa ukimwi kama Balozi wa Umoja wa Mataifa wa Shirika la Chakula.
Mreno huyo amesema kwamba anataka soka ifanye makubwa zaidi kusaidia mambo kama ambavyo WFP wanafanya, na akapendekeza FA ichangie faini inazokusanya kwenye mambo mazuri.
Mei mwaka huu, Mourinho alipigwa faini ya Pauni 10,000 na FA kwa kutoa maelezo yaliyowakera wakubwa kwenye vyombo vya habari dhidi ya marefa baada ya Chelsea kufungwa 2-1 na Sunderland, kipigo ambacho kilifanya rekodi yake ya kucheza mechi 77 bila kufungwa nyumbani izimwe.
0 comments:
Post a Comment