MCHUA misuli wa Luis Suarez aliahirisha kwenda kupatiwa matibabu ya saratani kuhakikisha mshambuliaji huyo wa Uruguay anakuwa fiti na kucheza dhidi ya England.
Walter Ferreira, mwenye umri wa miaka 63, alitarajiwa kwenda kufanyiwa tiba hiyo kabla ya Kombe la Dunia. Faida ya uamuzi wake wa kuahirisha zoezi hilo ilionekana Alhamisi wakati mabao mawili ya Suarez yalipoitupa nje ya Kombe la Dunia England.
Bao la kifo: Suarez akimtungua Joe Hart
Suarez, ambaye alimkimbilia Ferreira baada ya kuifungia Uruguay bao la kwanza la kuongoza, amekuwa akihudumiwa na mchua misuli huyo kwa wiki kadhaa zilizopita.
Ferreira alisema: "Nawashukuru benchi la ufundi liliniamini na kunipa kazi ya kumhudumia Luis.’
Majukumu: Ferreira alisitisha kwenda kufanyiwa tiba ya saratani ili amhudumie Suarez
Suarez alitoa shukrani zake kwa Ferreira kwa kumuwezesha kuwa fiti ndani ya muda na kucheza dhidi ya England, ambao amewarudisha nyumbani mapema.
"Kuna mtu ambaye alijua kiasi gani nilihitaji msaada wake. Kama si yeye (Ferreira) hata hapa nisingekuwepo. Nililia sana na yeye, kwa sababu ulikuwa wakati mgumu kiasi hicho, na wa kuchaganyanya kwa sababu amejitoa mhanga kubaki na mimi kwa muda wote,"amesema Suarez.
0 comments:
Post a Comment