MSHAMBULIAJI Robin van Persie ameendeleza makali yake kuelekea Kombe la Dunia baada ya usiku wa jana kufunga bao pekee Uholanzi ikiilaza 1-0 Ghana katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa De Kulp mjini Rotterdam.
Nyota huyo wa Manchester United alifunga bao zuri dakika ya tank akimalizia kazi nzuri ya kiungio Wesley.
Timu ya Louis van Gaal ilitawala mchezo mwanzo hadi mwisho na ingeweza kupata mabao zaidi kama si kupoteza nafasi ikiwemo ya Arjen Robben kabla ya mapumziko akiwa anatazama na lango.
Kikosincha Uholanzi kilikuwa: Cillessen, Janmaat, Vlaar, De Vrij, Martins Indi, Blind, De Jong, Sneijder/Lens dk81, De Guzman, Robben na Van Persie/Depay dk73.
0 comments:
Post a Comment