NDOTO za Nigeria kuungana na Cameroon, Senegal na Ghana katika orodha ya timu za Afrika zilizowahi kucheza Robo Fainali za Kombe la Dunia zimezimwa leo baada ya kufungwa mabao 2-0 na Ufaransa katika mchezo wa 16 Bora Uwanja wa Garrincha, Brasilia, Brazil.
Nigeria iliyotinga 16 kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998 baada ya kushika nafasi ya pili Kundi F, ilijitahidi kuwabana Ufaransa kwa muda mrefu, lakini ‘pumzi iliwakatika’ dakika za mwishoni.
Kabla ya Paul Pogba kufunga bao la kwanza kichwa dakika ya 79, kipa Vincent Enyiama alikoswa mabao matatu ya wazi, moja mchomo wa Karim Benzema ukiondolewa kwenye mstari wa lango na Victor Moses.
Beki Joseph Yobo naye akajifunga dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida, katika harakati za kuokoa krosi.
Kikosi cha Ufaransa kilikuwa: Lloris, Debuchy, Varane, Koscielny, Evra, Pogba, Cabaye, Matuidi, Valbuena/Sissoko dk90+4, Giroud/Griezmann dk62 na Benzema.
Nigeria: Enyeama, Ambrose, Yobo, Oshaniwa, Omeruo, Musa, Onazi/Gabriel dk59, Mikel, Moses/Nwofor dk89, Odemwingie na Emenike.
0 comments:
Post a Comment