UFARANSA imejihakikishia kiting 16 Bora ya Kombe la dunia baada ya kuichapa mabao 5-2 Uswisi katika mchezo wa Kundi E usiku huu mjini Salvador.
Mabao ya mabingwa hao wa 1998 yamefungwa na Olivier Giroud, Blaise Matuidi, Mathieu Valbuena, Karim Benzema na Moussa Sissoko.
Kikosi cha Didier Deschamps kilichofuzu kwa mbinde Kombe la Dunia, kingeondoka na ushindi mnene zaidi kama Benzema asingepoteza mkwaju wa penalti, baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na Stefan Lichtsteiner.
Heshima: Karim Benzema akishangilia baada ya kuifungia Ufaransa bao la tatu katika ushindi wa 5-2 dhidi ya Uswisi
Ufaransa sasa imetimiza pointi sita baada ya kucheza mechi mbili, ikifuatiwa na Uswisi yenye pointi tatu wakati Ecuador na Honduras zinazomenyana hivi sasa zote hazina pointi.
Kikosi cha Ufaransa kilikuwa; Lloris, Debuchy, Varane, Sakho/Koscielny dk66, Evra, Sissoko, Cabaye, Matuidi, Valbuena/Griezmann dk82, Giroud/Pogba dk63 na Benzema.
Kikosi cha Ufaransa kilikuwa; Lloris, Debuchy, Varane, Sakho/Koscielny dk66, Evra, Sissoko, Cabaye, Matuidi, Valbuena/Griezmann dk82, Giroud/Pogba dk63 na Benzema.
Uswisi; Benaglio, Lichtsteiner, Djourou, Von Bergen/Senderos dk4, Rodriguez, Inler, Behrami/Dzemaili dk46, Mehmedi, Xhaka, Shaqiri na Seferovic/Drmic dk69.
Mshambuliaji wa Real Madrid, Benzema akiangushwa chini na Stefan Lichtsteiner, lakini picha ya chini inamuonyesha akikosa penalti aliyoitengeza mwenyewe
0 comments:
Post a Comment