Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha wachezaji 26 cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kimeondoka lei (Juni 24 mwaka huu) alfajiri kwa ndege ya South African Airways kwenda Gaborone, Botswana ambapo kitapiga kambi ya wiki mbili.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeweka kambi hiyo chini ya Kocha Mart Nooij ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi yake ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika (AFCON) dhidi ya Msumbiji (Mambas) itakayochezwa Julai 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi kutoka Misri wakiongozwa na Mahmoud Ashor wakati Kamishna atakuwa Felix Tangawarima kutoka Zimbabwe.

0 comments:
Post a Comment