ANAWAPIKU Lionel Messi na Tim Cahill. James Rodriguez amefunga bao bora zaidi katika Kombe la Dunia hadi sasa kwa mwaka huu, akiiwezesha Colombia kuitoa Uruguay katika 16 Bora Uwanja wa Maracana.
Aliumiliki vizuri mpira wa kichwa katika kifua chake akiwa umbali wa mita 25 kutoka langoni, mvaa jezi mamba 10 huyo wa Colombia kisha akaushusha chini na akiwa amezingirwa na wachezaji wawili wa Uruguay, akafumua bonge la shuti hadi nyavuni.
0 comments:
Post a Comment