MASHABIKI wa Luis Suarez walijitokeza kwa wingi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Carrasco jirani na Montevideo kumlaki mshambuliaji huyo aliyefungiwa Kombe la Dunia akirejea nchini Uruguay.
Akiwa amefungiwa mechi tisa za kimataifa na miezi minne kwa ujumla kujihusisha na soka, Suarez alirejea Uruguay akiiacha timu yake imetinga Hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia.
Mashabiki walijimwaga mitaani hadi Uwanja wa Ndege kwenda kumpokea mshambuliaji huyo wa Liverpool nchini Uruguay, huku wengine wakiwa wamevaa picha yake kumtukuza nyota huyo.
Rais wa Uruguay, Jose Mujica alikuwas Uwanja wa Ndege pia kumpokea, lakini akaamua kuondoka katakana na ndege iliyokuwa inamrejesha Suarez kuchelewa.
Partisan: Supporters wanted to see the star striker arrive back in Uruguay following his ban
Shabiki akiwa ameshika bango la kuikandia FIFA kwa kumfungia Suarez
Shabiki mdogo akiwa na meno bandia mdomoni mwake Uwanja wa Ndege wa Carrasco
Watu wakiwa wamejipanga barabarani tayari kumpokea mshambuliaji huyo wa Liverpool
Barabara ya kuelekea Uwanja wa Ndege Carrasco watu wako tayari kwa mapokezi ya Suarez
Kwa sababu ya kuchelewa, umati wa watu wapatao 1,000 uliondolewa eneo la Uwanja wa Ndege na kuhamishiwa katika eneo la jeshi kuendelea kumsubiri Suarez awasili.
Mapema Suarez alipigwas picha akiwa na wachezaji wenake mjini Rio wakati wanawasili hotelini.
Uruguay itamenyana na Colombia katika 16 Bora ya Kombe la Dunia mechi ya timu za Amerika Kusini tupu.
0 comments:
Post a Comment