// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NDANDA FC WAWEKA NADHIRI MAPEMA LIGI KUU; “KILA ANAYEKANYAGA NANGWANDA SIJAONA NI KICHAPO TU” - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NDANDA FC WAWEKA NADHIRI MAPEMA LIGI KUU; “KILA ANAYEKANYAGA NANGWANDA SIJAONA NI KICHAPO TU” - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, June 20, 2014

    NDANDA FC WAWEKA NADHIRI MAPEMA LIGI KUU; “KILA ANAYEKANYAGA NANGWANDA SIJAONA NI KICHAPO TU”

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    WAGENI katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ndanda FC ya Mtwara wamesema kwamba hakuna timu itakayoweza kuvuna hata pointi moja kwenye Uwanja wao, Nangwnda Sijaona katika msimu ujao wa ligi hiyo.
    Katibu Mkuu wa Ndanda, Edmund Kunyengana Njowoka aliiambia BIN ZUBEIRY jana mjini Dar es Salaam kwamba timu yao tayari imeingia kambini kujiandaa na msimu ujao wa ligi hiyo.
    Njowoka amesema kwamba wamepania kufanya vizuri katika msimu ujao wa Ligi Kuu wakicheza kwa mara ya kwanza tangu wapande, lengo likiwa ni kurudisha heshima ya mkoa wa Mtwara na kuwapa raha wakazi wa mkoa huo.
    Edmund Kunyengana Njowoka kushoto, akiwa na Nassor Bin Slum jana

    “Sisi hatukuja kujaribu wala kubahatisha, tunawaambia kabisa hao wanaojiita vigogo, kwamba wasitegemee kuvuna pointi hata moja Mtwara,”alisema.
    Pamoja na yote Njowoka alikiri yeye ni mpenzi wa Yanga SC, lakini akasema mapema kwamba haimaanishi Ndanda litakuwa shamba la pointi Yanga.
    “Mimi ni Yanga damu, kila mtu anajua, lakini Yanga wakija Mtwara tunawachapa, wajue kabisa hivyo,”alisema. 
    Ndanda jana ilipata neema ya udhamini wa kampuni ya Bin Slum Tyres Limited, baada ya kusaini Mkataba wa mwaka mmoja, wenye thamani ya Sh Milioni 50.
    Bin Slum ambayo awali iliingia mikataba na Mbeya City ya Mbeya na Stand United ya Shinyanga, sasa inakuwa kampuni inayodhamini timu nyingi zaidi za Ligi Kuu, ikifuatiwa TBL, wanaozidhamini Simba na Yanga.
    Ndanda watavaa jezi zenye nembo ya matairi ya Vee Rubber kwa mbele pamoja na kuweka mabango ya bidhaa hizo kwenye mechi zao za nyumbani, Uwanja wa Nangwanda Sijaona.  
    Stand United pia wamepewa Mkataba wa Sh. Milioni kwa mwaka nao watavaa jezi zenye nembo ya matairi ya Double Star yanayosambazwa na kampuni ya Bin Slum katika mechi zake zote msimu wa 2014-2015.
    Mbeya City ambao watavaa jezi zenye nembo ya betri za RB zinazosambazwa na Bin Slum pia, wao wamepewa Mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh. Milioni 360.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NDANDA FC WAWEKA NADHIRI MAPEMA LIGI KUU; “KILA ANAYEKANYAGA NANGWANDA SIJAONA NI KICHAPO TU” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top