// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIUNGO MPYA MBRAZIL WA YANGA AKWAMA KUJA NA MAXIMO KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIUNGO MPYA MBRAZIL WA YANGA AKWAMA KUJA NA MAXIMO KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, June 26, 2014

    KIUNGO MPYA MBRAZIL WA YANGA AKWAMA KUJA NA MAXIMO KESHO

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KIUNGO mpya Mbrazil wa Yanga SC, Andrey Coutinho hataweza kuja kesho pamoja na makocha Marcio Maximo na Leonardo Neiva Martins baada ya kushindwa kukamilisha taratibu za safari mapema.
    Maximo na Leonardo wanatarajiwa kutua kesho mchana na ndege ya shirika la Afrika Kusini, lakini baada ya uongozi wa Yanga SC kuwatumia tiketi haukupata mawasiliano nao kuhakikisha kama wamekamilisha taratibu za safari.
    Andrey Coutinho amekwama kukamilisha taratibu za safari mapema kuja Dar es Salaam kujiunga na Yanga

    Coutinho aliuarifu uongozi wa Yanga juu ya kushindwa kukamilisha taratibu za safari mapema, lakini kwa kuwa Maximo na Leonardo hawajasema chochote- maana yake mambo safi na kesho wanaweza kutua Dar es Salaam.
    Coutinho sasa anatarajiwa kutua nchini kuanzia Ijumaa.  
    Yanga SC imeajiri Wabrazil hao wote watatu ili kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao, kiweze kurejesha heshima yake baada ya msimu huu kupokonywa ubingwa wa Ligi Kuu na Azam FC ya Dar es Salaam pia.
    Maximo ni kocha ambaye amekuwa kwenye rada za Yanga SC kwa muda mrefu, tangu alipoachana na timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars miaka minne iliyopita, wakati Leonardo anakuja kuwa Msaidizi wake.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIUNGO MPYA MBRAZIL WA YANGA AKWAMA KUJA NA MAXIMO KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top