• HABARI MPYA

        Tuesday, June 24, 2014

        ITALIA NJE KOMBE LA DUNIA, SUAREZ ANG'ATA MTU TENA, ENGLAND YAAMBULIA POINTI BRAZIL

        ITALIA imeaga Kombe la Dunia nchini Brazil baada ya kufungwa 1-0 na Uruguay, bao pekee la Diego Godin katika mchezo ambao mshambuliaji Luis Suarez alimng’ata Giorgio Chiellini.
        Godin alifunga bao hilo dakika ya 81 na kipa Buffon wa Italia alilazimika kuingia uwanjani dakika ya mwisho kusaidia nguvu ya kusaka bao, Azzuri ikihtaji sare tu kusonga mbele.
        Italia ilimpoteza mchezaji wake Marchisio aliyetolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Arevalo Rios dakika ya 60.
        Mkongwe wa Italia, Andrea Pirlo (kushoto) akibadilishana jezi na Edisnon Cavani wa Uruguay baada ya mechi

        Suarez baada ya kumng'ata Chiellini
        Refa hakumpa adhabu Suarez
        Chiellini akilalamika kung'atwa na Suarez begani
        Costa Rica imemaliza kileleni mwa Kundi D baada ya sare ya 0-0 na England leo ikifikisha pointi saba, Uruguay pointi sita na Italia pointi tatu, wakati England imeondoka na pointi moja.
        Kikosi cha Italia kilikuwa; Buffon, Barzagli, Bonucci, Chiellini, Marchisio, De Sciglio, Verratti/Motta dk75, Pirlo, Darmian, Balotelli/Parolo dk46 na Immobile/Cassano dk71.
        Uruguay: Muslera, Caceres, Gimenez, Godin, A.Pereira/Stuani dk63, Gonzalez, Arevalo Rios, Rodriguez/Ramirez dk78, Lodeiro/M Pereira dk46, Cavani na Suarez.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: ITALIA NJE KOMBE LA DUNIA, SUAREZ ANG'ATA MTU TENA, ENGLAND YAAMBULIA POINTI BRAZIL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry