KIUNGO Ander Herrera amekamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 29 kwenda Manchester United akitokea Athletic Bilbao.
Klabu hiyo ya La Liga ilikataa ofa ya timu hiyo ya kocha Louis van Gaal, lakini baada ya mchezaji huyo kufuzu vipimo vya afya Carrington jana, dili hilo limekamilishwa.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 sasa anakuwa mchezaji wa kwanza kabisa kusajiliwa na Man United chini ya kocha mpya, van Gaal aliyerithi mikoba ya David Moyes Old Trafford.
Kimeelewekal: Herrera akiwa ameshika jezi ya Man United pamoja na Sir Bobby Charlton baada ya kukamilisha uhamisho wake
0 comments:
Post a Comment