Na Samira Said, DAR ES SALAAM
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Simba, Hassan Daalal, amewataka wanachama wa klabu hiyo wampe kura Evans Aveva kwa sababu ndio kiboko ya Yanga.
Dalali amewaambia wanachama wa Simba Wilaya ya Kinondoni waliohudhuria katika mkutano wa kampeni uliofanyika jioni hii kwenye ukumbi wa Urafiki Hall, Ubungo.
Alisema kuwa wanachama wakimchagua Aveva basi watafurahi msimu mzima kama mgombea huyo alipokuwa anaongoza kamati ya usajili ya klabu hiyo.
Daalal pia alimtaka Aveva pia kudumisha umoja ndani ya Simba na hakuna kinachofanikiwa kama watu hawashirikiani.
Alimtaka mgombea huyo akifanikiwa kuingia madarakani kukutana na viongozi wa matawi ambao ndio wanasaidia kufanikisha pointi tatu muhimu.
"Tutumie nguvu zetu na utu wetu kurudisha heshima ya Simba", alisema Daalal.
Pia amemtaka mgombea huyo akishinda afanye kikao pia na wazee ambao katika kipindi cha uongozi uliopita hawakushirikishwa.
Alisema pia anasikitika kuona mashabiki wanashindwa kujitokeza uwanjani kuhudhuria mechi zao kwa kuogopa kufungwa na hatimaye klabu yao kuingiza Sh 200,000 kiasi ambacho ni kidogo na hakifanani na hadhi ya Simba .
Alisema baada ya kikao hiko wataelekea Bagamoyo na kesho Jumamosi wataelekea Zanzibar kuwaomba radhi wazee wa huko warejee na kuisaidia klabu ipate mafanikio. "Mpeni Evans Aveva", alisema Daalal. Uchaguzi wa Simba unatarajiwa kufanyika Jumapili.

Mzee Daalal amewomba wana Simba wamchague Aveva |

0 comments:
Post a Comment