WACHEZAJI ndugu, Yaya na Kolo Toure wamepokea taarifa ya msiba wa mdogo wao, Toure Oyala Ibrahim wakati wakiwa na timu yao ya taifa, Ivory Coast kwenye Kombe la Dunia Brazil.
Mdogo huyo wa nyota hao wa Manchester City na Liverpool, amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 28 jana mjini Manchester baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani- saa kadhaa baada ya ndugu zake kushiriki kwenye kikosi cha Ivory Coast kilichofungwa mabao 2-1 na Colombia.
Shirikisho la Soka Ivory Coast limewapa pole Yaya na Kolo juu ys msiba wa ndugu yao aliyekuwa mchezaji pia, huku timu hiyo iliyo Kundi C ikiomba dua za wananchi wa Ivory Coast katika wakati huu mgumu.
WASIFU WA TOURE OYALA IBRAHIM
2002-2003: ASEC Mimosas
2003-2006: Metalurh Donetsk
2006-2007: OGC Nice
2009-2010: Al-Ittihad Aleppo
2010-2013: Misr Lel Mikasa
2012: Telephonat Beni Sweif (loan)
2013-2014: Al-Safa' SC
Inafahamika Ibrahim alikuwa akipatiwa matibabu ya marathon yake hayo katika hospitali ya The Christie, na Yaya alikuwa akimtembelea ndugu yake hayo kila siku.
Manchester City ni miongini mwa waliotoa salami za rambirambi ya msiba wa tributes to Ibrahim.
"Fikra za kila mmoja katika Manchester City FC zipo kwa Yaya na Kolo Toure kufuatia lifo cha mdogo wao, Ibrahim,"imesema taarifa ya klabu hiyo.
"Ibrahim alikuwa mgeni wa kawaida Carrington na alikuwa maarufu mbele ya viongozi na wachezaji na kwa hakika alikuwa karibu sana na kaka zake,".
0 comments:
Post a Comment