Na Prince Akbar, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Soka Marocco (FRMF) limemteua kipa wake wa zamani wa kimataifa, Badou Zaki kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Simba wa Atlasi kwa mara ya pili, akichukua nafasi ya Hassan Benabicha, aliyekuwa anakaimu nafasi hiyo.
Gwiji huyo mwenye umri wa miaka 55, ambaye awali alipewa timu hiyo kati ya mwaka 2002 na 2005, ataiongoza Morocco kwenye Fainali zijazo za Mataifa ya Afrika, mwakani ambazo nchi hiyo ya Kaskazini mwa bara hili ni mwenyeji.
Rais wa FRMF, Fouzi Lekjaa ametangaza uteuzi huo katika Mkutano na Waandishi wa Habari jana mjini Rabat. Badou alikuwemo kwenye kikosi cha Simba wa Atlasi kilichofuzu kutoka hatua ya makundi ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1986, hiyo ikiwa ni ya mara ya kwanza kwa timu ya Afrika kuvuka hatua hiyo, mwaka ambao pia alishinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Afrika.
Amecheza fainali nne za Mataifa ya Afrika katika miaka ya 1980, 1986, 1988 na 1992. Pia alizitumikia klabu za AS Sale, Wydad Athletic Club, FUS Rabat na akaichezea kwa miaka sita, Real Mallorca ya Hispania.
Atakuwa anasaidiwa na wachezaji wenzake wa zamani wa kimataifa wa nchi hiyo, Mustapha Hadji na Said Chiba wakati Khalid Fouhami atakuwa kocha wa makipa na Aziz Bouderbala atakuwa Mratibu wa timu.

Bosi mpya; Badou Zaki amerejeshwa kuinoa Morocco |

0 comments:
Post a Comment