DEREVA wa Formula One, Nico Rosberg na wachezaji wawili wa kikosi cha Ujerumani cha Kombe la Dunia wamepata ajali pamoja wakati wa kuchukua picha za promosheni katika kambi yao ya mazoezi Jumanne, ambayo ilifanya watu wawili wakimbizawe hospitali.
Rosberg na dereva wa DTM, Pascal Wehrlein walikuwa wamewabeba wachezaji wa Ujerumani, Julian Draxler na Benedikt Howedes katika gari tofauti wakati gari la Wehrlein lilipowagonga watu wawili barabarani kaskazini mea Italiia, South Tyrol. Barabara hiyo ilikuwa imefungwa kwa matumizi ya umma.
"Nimeshitushwa na ajali hii,"alisema Rosberg, ambaye anaongoza michuano ya ubingwa wa dunia ya Formula One baada ya kushinda Jumapoli mjini Monaco katika mbio za Grand Prix.
Uchunguzi: Polisi wa Italia walifunga barabra hiyo baada ya ajali hiyo iloyotokea karibu na kambi ya mazoezi ya timu ya taiga ya Ujerumani mjini San Martino
Wachezaji wa kimataifa wa Ujerumani, Benedikt Howedes (kushoto) na Julian Draxler wote walihusika katika ajali
Ujerumani imeweka kambi ya maandalizi ya Kombe la Dunia katika hotel ya Alpine kaskazini mwa Italia tangu wiki iliyopita na itaendelea kuwa huko hadi Juni 1.
0 comments:
Post a Comment