KOCHA mpya wa Manchester United, Louis van Gaal amewaondoa Cesc Fabregas na Toni Kroos katika orodha ya wachezaji anaotaka kuwasajii msimu ujao na kuelekeza nguvu zake kwa wachezaji wengine akiwemo mpachika mabao wa Bayern Munich, Bastian Schweinsteiger.
Mholanzi huyo amesema kwamba, ana matumaini kocha wa Munich, Pep Guardiola atakuwa tayari kusikiliza ofa ya Pauni Milioni 10 kwa ajili ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29.
Schweinsteiger, ambaye jina lake lilitajwa pia wakati wa David Moyes akiwa kazini United, pia ana nia ya kwenda kukabiliana na changamoto mpya.
Anamuhitaji: Bastian Schweinsteiger anaweza kupatikana kwa dau la Pauni Milioni 10 na Van Gaal anamuhitaji kiungo huyo
Pia Van Gaal anawataka beki wa kulia wa Feyenoord, Daryl Janmaat, beki wa kati Bruno Martins Indi na beki wa Ajax, Daley Blind na mpango wa kumsajili Kevin Strootman wa AS Roma bado upo, mara itakapothibitika anaweza kupona maumivu yake goti.
Wakati huo huo, Danny Welbeck amesema amevurugwa kwa kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha United msimu uliopita, kwani mshambuliaji huyo wa England anataka kupangwa katikati athibitishe uwezo wake wa kufunga kwa kiwango cha juu katika klabu na timu ya taifa.
Welbeck amefunga mabao manane katika mechi 21 za timu ya taifa, lakini alikuwa akisotea namba kikosi cha kwanza chini ya David Moyes United.
0 comments:
Post a Comment