IKICHEZA bila mshambuliaji wake nyota, Luis Suarez ambaye ni majeruhi kwa sasa, Uruguay jana iliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ireland Kaskazini katika mchezo wa kujiandaa na Kombe la Dunia.
Ushindi huo umetokana na bao pekee la Christian Stuani aliyetokea benchi ambaye aliwamalzia Ireland Kaskazini.
Mchezaji huyo aliingia uwanjani kuchukua nafasi ya mkongwe, Diego Forlan aliyeongezwa kikosini baada ya kuumia kwa Suarez.
0 comments:
Post a Comment