TUNAINGIA sehemu ya nne na ya mwisho ya makala haya ya takafuri ya kina ndani ya klabu ya Yanga SC, tangu ikiwa chini ya Mwenyekiti marehemu Tarbu Mangara hadi Wakili Lloyd Baharagu Nchunga aliyeupisha uongozi wa sasa chini ya Mwenyekiti, Yussuf Manji je- ni wakati upi klabu hiyo ilipitia mikononi mwa viongozi bomu zaidi.
Katika sehemu ya tatu tulitazama utendaji na matokeo ya uongozi unaomaliza muda wake hivi sasa chini ya Mwenyekiti Manji. Endelea.
Yanga SC inaitwa klabu kubwa, haina hata Uwanja wa mazoezi- Manji na utajiri wake na hao matajiri wenzake wake wameshindwa kununua hata eneo la Sh. Milioni 20 nje ya miji ambayo wananchi wa kawaida wanaunua kila siku, klabu ikapata Uwanja?
Hawa mawakili Madega na Nchunga walioiongoza Yanga SC katika vipindi viwili vilivyopita walikuwa wana akili na dhamira nzuri kwa klabu hiyo, lakini wote walitofautiana na mfadhili. Sielewi kwa nini wazo la kuifanya Yanga SC ijitegemee limekuwa kosa la jinai tangu enzi.
Reginald Mengi alikuwa mtu wa kwanza kuwasilisha wazo hilo Yanga SC na akaahidi kutoa msaada mkubwa ili klabu ifanikiwe kuwa kampuni, lakini alipata upinzani mkubwa kwa waliokuwa wafadhili wa klabu hiyo wenye asili ya Kiasia.
Mwishowe Mengi alijiweka kando- na hata akina Tarimba Abbas, Francis Kifukwe, Abdul Sauko na Jamal Malinzi waliorejea na wazo hilo baadaye, nao wote walichemsha na kuachia ngazi baada ya kupigwa vita kubwa.
Hakika uongozi wa Manji ulibeba matumaini ya wana Yanga SC kwa kiasi kikubwa, kwa sababu hata nao wazo lao lilikuwa kuanzisha kampuni ya hisa, lakini wanamaliza muda wao bila chochote cha maana.
Kushinda ubingwa wa Ligi Kuu si jambo geni, Yanga SC ilifanya hivyo Mwenyekiti Ngozoma Matunda na kocha Tito Mwaluvanda (wote marehemu), sembuse leo Mwenyekiti bilionea Manji na makocha Wazungu mfululizo.
Yanga SC inahitaji mageuzi ya kiuchumi na mfumo mzima wa uendeshwaji kwa ujumla, ili mashabiki wake wafurahie mafanikio ya ndani na nje ya Uwanja badala ya kuendelea kuwa klabu ambayo mtu akinuna hapaliki, hapakaliki.
Manji ni tajiri, msomi na kijana mdogo mbunifu, lakini mambo ya mpira inaonekana yamempita kushoto kidogo, Clement Sanga naye ndiyo hivyo, hao wengine wanaojifanya wajuaji walishindwa kusimamia vitimu vidogo kama Moro United visivyo na presha yoyote, hapo ungetegemea nini.
Kwa makosa yao wenyewe, waliwaadhibu na kuwadhalilisha watu wengine mfano kocha Mbelgiji Tom Saintfiet, Katibu Celestine Mwesigwa na Ofisa Habari, Louis Sendeu eti wakataka hadi kuwavua uanachama, wakati wao uanachama wao ni wa juzi juzi na mapenzi yao kwa Yanga yanatia shaka.
Huo ni ubinafsi mbaya waliouingiza kwenye klabu- wakapeana majukumu mtoto wa mjomba kwa shangazi na kwa sababu Manji hana muda wa kufuatilia na Sanga hana nguvu kwao, basi Yanga SC ilifanywa kama timu ya ukoo na matokeo yake ndiyo haya.
Mwesigwa ameonyesha ni mtu mweledi, baada ya kuajiriwa kama Katibu TFF, hajatumia nafasi hiyo kulipa kisasi, angetaka angeweza- kwanza kwenye suala la utata tu wa usajili wa Emmanuel Okwi.
Lakini alitoa ushirikiano kwa kupeleka barua FIFA ili itoe ridhaa ya mchezaji huyo kucheza- ila kuna watu ndani ya Yanga SC kila kukicha wanaijengea uadui klabu dhidi ya watu na taasisi mbalimbali, na wanachama wamenyamaza, lakini mwisho wa siku hao watu wataondoka na itakayonufaika au kuumia ni klabu.
Mtu anaamka na mawazo yake aliyoshauriana na mkewe, anakwenda kwa Manji kuchukua fedha anafanya usajili, bila kushirikisha wenzake japo wa Kamati ya Utendaji tu.
Kwa nini nauliza umewahi kutokea uongozi bomu kuliko huu Yanga SC- ni kwa sababu kama hizi, mtu mmoja anaweza kuamua bila kushirikisha wengine ndani ya uongozi, na ambao hawakushirikishwa wasiseme lolote.
Klabu kutumia fedha nyingi katika usajili usiozingatia vigezo vya kitaalamu, kuweka kambi za gharama kubwa Uturuki bila kuzingatia ushauri wa kitaalamu na kutojali kuhusu maslahi ya wachezaji.
Kushindwa kuitengenezea klabu mustakabli mzuri na matokeo yake taswira ya makao makuu ya klabu imezidi kuharibika- kwa ujumla kushindwa kutekeleza ahadi, achilia mbali kuendelea kuwa timu dhaifu mbele ya watani, Simba SC.
Manji amekwishasema hagombei, na je akiwa nje ya klabu ataendelea kumwaga fedha zake? Hilo moja, pili TBL ikisitisha udhamini wake, Yanga SC itategemea chanzo kipi kingine cha mapato zaidi ya fedha za milangoni kwenye mechi?
Yanga SC mwenye akili anaweza kunielewa kwa urahisi sana, lakini mbumbumbu na mamluki hatanielewa daima na atanichukia milele.
Yanga SC ni mwenye nyumba pekee ambaye hanufaiki na nyumba zake- si kwa yeye mwenyewe kuishi au kuweka wapangaji.
Mbeya City timu mpya, lakini inauza jezi na inakusanya mapato ya jezi, siku Yanga inacheza Uwanja wa Taifa mashabiki wanafanana na wachezaji wao kwa jezi uwanjani, tena zenye nembo ya klabu, lakini ajabu klabu haipati hata senti moja na jezi hizo zinauzwa wazi wazi.
Unapozungumzia namna ya Yanga SC kunufaika na rasilimali watu ni kuuza bidhaa kama hizo zenye nembo ya klabu, kama jezi, kofia, fulana, vitopu vya mabindi na mapambo mengine yakiwemo ya kwenye magari.
Yanga SC inaweza kufanya hivyo hata kwa kuingia ubia na makampuni ambayo yanatengeneza bidhaa hizo na ikanufaika- lakini kwa kuwa akili za viongozi wao hazijalalia huko, basi shamba la bibi, kila mjukuu ana haki kujivunia. Alamsiki.

0 comments:
Post a Comment