Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
TANZANIA imeendelea kung’ang’ara kwenye Michezo ya Afrika kwa Vijana (AYG) kwa upande wa mpira wa miguu kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 baada ya jana (Mei 25 mwaka huu) kuichapa Swaziland mabao 3-0.
Mabao ya Tanzania katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Gaborone, Botswana yalifungwa na Amani Ally dakika ya sita, Nasson Chanuka dakika ya 32 wakati Amos Kennedy alikamilisha ushindi huo kwa bao la dakika ya 53.
Katika mechi yake ya kwanza, Tanzania ilitoka sare ya bao 1-1 na Mali na baadaye kuwafunga wenyeji Botswana mabao 2-0.
Baada ya U20 kutolewa mapema michuano ya Afrika, Watanzania wanajifariji kupitia U15 yao inayofanya vizuri Botswana |
Mechi za michuano hiyo zinaoneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini.
Tanzania itacheza mechi yake ya nne kesho (Mei 27 mwaka huu) dhidi ya Nigeria wakati mechi ya mwisho itafanyika Mei 29 mwaka huu dhidi ya Afrika Kusini.
0 comments:
Post a Comment