MSHAMBULIAJI Fernando Torres jana amefunga bao Hispania ikishinda 2-0 dhidi ya Bolivia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki kujiandaa na Kombe la Dunia.
Mshambuliaji huyo wa Chelsea alifunga bao hilo kwa penalti akimtungua kipa Romel Quininez dakika ya 51 na Andres Iniesta akafunga la pili dakika ya 81.
Kikosi cha Hispania kilikuwa: Reina, Moreno, Azpilicueta, Pique/Albiol, dk46, Xavi/Busquets, dk61, Martinez, Cazorla/Silva, dk62, Iturraspe, Pedro/Deulofeu, dk80, Mata/Iniesta, dk46 na Torres/Fabregas, dk62.
Bolivia: Quinonez, Bejarano, Raldes/Zenteno, dk90, Melean/Miranda, dk64, Eguino. Gutierrez, Chumacero/Da. Bejerano, dk64, Di. Bejarano, Mojica/Cardozo, dk72, Arce/Arze, dk72 na Moreno/Pena, dk82.
0 comments:
Post a Comment