Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
MTANZANIA anayechezea klabu ya SPBGG 1914 Selbitz ya Ujerumani, Charles Mishetto ameendelea kung’ara baada ya jana kufunga bao moja timu yake ikilala 2-1 mbele ya SVO 1912 ugenini.
Katika mchezo huo Ligi Daraja la Nne, iitwayo Bayernliga 4, Michael Johnson aliwafungia wenyeji dakika ya 10 na Ricko Muller akafunga la pili dakika ya 26, kabla ya Mishetto kuifungia Selbitz dakika ya 62.
Mishetto aliangushwa kwenye eneo la hatari na timu yake ikapewa penalti, lakini bahati mbaya yeye mwenyewe akakosa. “Nimekosa penalti, kwa bahati mbaya, ila nimefunga bao moja na nilicheza vizuri, nimepongezwa,”alisema Mishetto baada ya mechi akizungumza na BIN ZUBEIRY kutoka Ujerumani.
Mwishoni mwa wiki, Mishetto alisema anataka kurudi nyumbani kucheza kwa msimu mmoja ili kujitangaza kabla ya kurejea tena Ulaya.
Mshambuliaji huyo wa timu hiyo ya Jijini Munich amesema kwamba anataka kuja nyumbani kucheza ili aonyeshe uwezo wake aweze kuitwa timu ya taifa na baada ya hapo wakala wake atamrudisha Ulaya.
“Najua njia pekee ya kuonekana nacheza nyumbani na watu kunijua na kuujua uwezo wangu ni kucheza timu ya taifa, na ili nicheze timu ya taifa lazima nionekane nacheza nyumbani,”alisema.
Mishetto anayechezea timu ya Daraja la Nne Ujerumani amesema kwamba anaamini akipata timu Tanzania ataitwa timu ya taifa, kwa sababu anaamini juu ya uwezo wake.
“Mtu akisikia ligi daraja la nne anaweza kudharau, lakini ni ligi moja yenye ushindani na ngumu, pengine kuliko ya huko nyumbani. Ndiyo maana nataka nije huko nicheze watu waone uwezo wangu,”alisema.
Mishetto ameomba timu itakayoonyesha nia ya kumsajili iwasiliane BIN ZUBEIRY ambayo itaunganisha mawasiliano baina yao.

Charles Mishetto chini kushoto na juu takwimu za mechi zikimuonyesha amefunga dakika ya 62 jana |

0 comments:
Post a Comment