MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Alexis Sanchez alitengeneza mabao tote matatu Chile ikitoka nyuma kwa 2-0 dhidi ya Misri na kushinda 3-2 jana katika mchezo wa kujiandaa na Kombe la Dunia.
Chilea ambayo itacheza na Australia katika mchezo wao nwa kwanza wa Kombe la Dunia Juni 13, ilipigwa mabao mawili ya haraka ya mashambulizi ya kushitukiza yaliyotiwa kimiani na Mohamed Salah dakika ya 12 na Khaled Kamr dakika nne baadaye.
Baada ya hapo, Sanchez akawasetia Marcelo Diaz dakika ya 26 na Eduardo Vargas aliyefunga mawili dakika ya 30 na 78.
0 comments:
Post a Comment