MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo alikosa mazoezi ya Ureno jana na atakosa mchezo wa kirafiki leo dhidi ya Ugiriki baada ya kulalamika maumivu ya misuli ya mguu wake wa kushoto, amesema kocha Paulo Bento jana.
Bento hafikiri kama kutakuwa na tatizo kumkosa Ronaldo katika mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Dunia dhidi ya Ujerumani, lakini amesema anahitaji kupona haraka kuwahi mechi zitakazofuatia.
Ronaldo alijiunga na kikosi cha Ureno Alhamisi wiki hii pamoja na nyota wenzake wa Real Madrid, Pepe na Fabio Coentrao katika kambi ya timu yao, hoteli ya Obidos.
0 comments:
Post a Comment