BAO la Bobby Zamora dakika ya 89 na sekunde 50 limeirejesha Ligi Kuu ya England QPR baada ya kuifunga 1-0 Derby Count katika fainali ya Ligi Daraja la Kwanza, maarufu kama Championship.
Baada ya kutaliwa na kikosi cha makinda cha Steve McClaren, mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 33 alionyesha tofauti ya watoto na watu wazima kwa boa hilo la dakika ya 89 na sekunde ya 50.
Nahodha wa County, Richard Keogh alishindwa kuondosha mpira kwenye eneo la hatari na kumpa nafasi mkongwe huyo kuukuta na kuusukumia nyavuni pembezoni mwa lango.
Wamerudi; QPR wamerejea Ligi Kuu ya England kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Derby Count leo |
Mshindi wa mechi: Bobby Zamora amefunga bao la jshindi linaloirejesha QPR Ligi Kuu
0 comments:
Post a Comment