// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PIGO MAN UNITED NA VAN GAAL, KROSS ASEMA ANABAKI BAYERN MUNICH NA MAN UNITED SIYO ISHU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PIGO MAN UNITED NA VAN GAAL, KROSS ASEMA ANABAKI BAYERN MUNICH NA MAN UNITED SIYO ISHU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, May 23, 2014

    PIGO MAN UNITED NA VAN GAAL, KROSS ASEMA ANABAKI BAYERN MUNICH NA MAN UNITED SIYO ISHU

    KIUNGO Toni Kroos hana mango wa kuhamia Manchester United msimu ujao. 
    Kiungo huyo wa Bayern Munich amekuwa akitakiwa kwa muds mrefu na klabu hyo ya Old Trafford, hususan wakati ambao suala la mkataba wake halijatatuliwa na mabingwa hao wa Ujerumani. 
    Kroos, mwenye umri wa miaka 24, amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na Bayern na bado hawajaafikiana juu ya mkataba mpya, jambo linajenga uwezekano wa kuondoka. 
    Tabasamu la furaha: Toni Kroos akiwa mazoezini na timu ya taiga ya Ujerumani jana, mchezaji huyo anaamini atabaki Bayern Munich msimu ujao

    Kroos yupo kwenye mipango ya kocha wa Manchester United, Louis van Gaal ambaye amewahi kufanya nays kazi Bayern lakini amesema vigogo hao wa England hawapo katika rada zake. 
    "Natarajia kuichezea Bayern Munich msimu ujao. Kumekuwa na tetesi nyingi, lakini Manchester haikuwa na haitakuwa ishu. Kwa wakati huoo, fikra zangu zone zipo kwenye maandalizi ya Kombe la Dunia,".
    Kroos alitarajiwa kuhamia Man United kwa Pauni Milioni 20 baada ya klabu hizo mbili kufikia makubaliano wakati David Moyes bado yupo kazini. 
    Wakati huo huo, Rais wa Bayern, Karl Hopfner, amesema Kroos yuko mbioni kupata Mkataba mpya mzuri kutuoka kwa mabingwa hao wa Ujerumani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PIGO MAN UNITED NA VAN GAAL, KROSS ASEMA ANABAKI BAYERN MUNICH NA MAN UNITED SIYO ISHU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top