UFARANSA imeanza maandalizi yake ya Kombe la Dunia Brazil mwezi ujao kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Norway jana usiku Uwanja wa Stade de Frane.
Mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud alifunga mabao mawili mazuri dakika za 50 na 68, wakati Paul Pogba wa Juventus alifunga dakika ya 15 na Loic Remy dakika ya 67.
Mabingwa hao wa Kombe la Dunia mwaka 1998, wamepangwa Kundi E pamoja na Ecuador, Usiwsi na Honduras.
0 comments:
Post a Comment