Na Renatus Mahima, Mbeya
KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooij ametangaza kipindi cha siku 14 za hatari kwa wachezaji wa kikosi hicho kwa kuwa kutakuwa na mazoezi makali ndani ya kipindi hicho kabla ya kuwakabili Zimbabwe.
Nooij aliyepewa mkataba wa miaka miwili kuinoa Stars na Shirikisho la Soka nchini (TFF) ataiongoza timu hiyo kusaka tiketi ya kufuzu kwa fainali za Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Akizungumza mara tu baada ya mechi ya kimataifa ya kirafiki waliyotoka suluhu na Malawi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini hapa juzi, Nooij alisema kikosi chake kitakuwa na mazoezi makali ili kujiweka vizuri kabla ya mechi yao ya kwanza dhidi ya Zimbabwe itakayopigwa kwenhye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kati ya Mei 16 na 18 mwaka huu.
“Tumepata kipimo kizuri katika mechi ya leo (juzi), ilikuwa nzuri na tulijitahidi kusaka magoli lakini wapinzani wamecheza kwa kujihami. Sasa tuna siku 14 ambazo zitakuwa hatari kwetu kwa sababu tunahitaji kufanya mazoezi magumu na makali," alisema Nooij
“Nimebakiwa na siku 14 ya kuwanoa wachezaji wangu kabla ya kupambana na Zimbabwe, hivyo nitawapa mazoezi ya nguvu kwa siku hizo ili kuwaimarisha, kwani mechi ya Zimbabwe ni ngumu sana kama hii ya Malawi,” alisema Nooij.
Naye kocha msaidizi wa Malawi, Jack Chamangwana aliipongeza Stars kwa kuonesha kandanda safi, huku akieleza kuwa alizuia muda mwingi wa mchezo kwa kuwa yuko ugenini.
“Kikosi change kinaundwa na wachezaji wa Ligi ya Malawi kuna wachezaji wanne wanaocheza nje ya nchi naamini nikiwachangabya na hawa nitapata kikosi bora zaidi kwa ajili ya kucheza na Chad kuwania kushiriki AFCON,” alisema Chamangwana.
Hiyo ni mechi ya pili kwa Nooij kuishuhudia Stars baada ya kuwepo jukwaani wakati Stars ikifungwa mabao 3-0 dhidi ya Burundi kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, hiyo ilikuwa masaa machache baada ya kuingia mkataba wa miaka miwili ya kuinoa timu hiyo.

Mart Nooij kushoto akiiongoza Stars kwa mara ya kwanza juzi mjini Mbeya |

0 comments:
Post a Comment