// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NOOIJ AANZA KWA SARE STARS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NOOIJ AANZA KWA SARE STARS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, May 04, 2014

    NOOIJ AANZA KWA SARE STARS

    Na Renatus Mahima, Mbeya
    KOCHA mpya wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Mart Nooij kutoka Uholanzi, leo ameanza kwa sare ya bila kufungana na Malawi katika mchezo wa kirafiki uliofanyika jioni hii Uwanja wa Sokoine mjini hapa. 
    Timu zote zilicheza sawa mechi hiyo wageni wakianza kwa kasi, lakini baadaye wenyeji wakawatuliza na kuanza kupokezana mpira.
    Aaanza na sare; Kocha mpya wa Taifa Stars,Mart Nooij ameanza na sare leo

    Dakika ya 23 mshambuliaji wa Malawi, Ndaziona Chatsalira alifumua shuti kali lakini kipa wa Tanzania Deo Munishi ‘Dida’ akapangua na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.
    Winga hatari wa Yanga SC, Simon Msuva alikosa bao la wazi dakika ya 41 baada ya kupiga nje akiwa ndani ya sita.
    John Bocco aliambaa vizuri na mpira dakika ya 66 hadi ndani ya boksi la Malawi, lakini shuti lake la mguu wa kulia likagonga mwamba wa lango na kurudi uwanjani.
    Beki wa Malawi John Banda alionywa kwa kadi ya njano dakika ya 75 baada ya kumkwatua kiungo wa Tanzania, Amri Kiemba.  
    Douglas Chirambo wa Malawi alikosa bao la wazi akiwa amebaki na kipa wa Tanzania, Deo Munishi ‘Dida’.
    Baada ya mechi hiyo, Mholanzi kocha Nooij aliyerithi mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen mwezi uliopita, alisema ni mwanzo mzuri na sasa anaingia kwenye mchakato wa kuboresha kikosi.
    Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi alisema kwamba atazungumza na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kuwashawishi waukubali Uwanja wa Sokoine kutumika kwa mechi za kimataifa.
    Uwanja wa Sokoine ni wa kihistoria ukiwa umewahi kutoa bingwa wa Bara,Tukuyu Stars mwaka 1986 na timu tishio kama Mecco, Tiger enzi hizo pamoja na Prisons na Mbeya City zinazotamba katika Ligi Kuu hivi sasa.
    Kikosi cha Tanzania leo kilikuwa; Deogratius Munishi ‘Dida’, Erasto Nyoni/Himid Mao dk70, Oscar Joshua, Aggrey Morris, Nadir Haroub ‘Cannavaro’,  Shomary Kapombe, Frank Domayo/Kevin Friday dk78, Amri Kiemba, Simon Msuva/Haroun Chanongo dk73, John Bocco na Ramadhani Singano ‘Messi’/Khamis Mcha dk81.
    Malawi; Charles Siwini, Bashiri Maunde, Emmanuel Zoya, Young Chimodzi Jr, John Banda, Rodrick Gonani, Frank Banda, Gaston Simukonda, George Nyirenda, Ndaziona Chatsalira na John Lanjesi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NOOIJ AANZA KWA SARE STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top