MGOGORO umeibuka kuhusu tarehe ya pambano baina ya bondia bora zaidi duniani, Floyd Mayweather na Amir Khan kwa sababu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ambalo limepangwa kufanyika Mei mwakani.
Khan amesema: "Siwezi kuwa tayari kwa tarehe hiyo. Ramadhani haimaliziki hadi mwishoni mwa Julai na ningependa nipate miezi mitatu ya kuwa kambini baada ya hapo, kujiandaa na pambano la aina yake. Kurudi mapema zaidi ulingoni ni mwishoni mwa Oktoba au mwanzoni mwa Novemba na hapo itabidi nipate mpinzani mwingine.
"Nimemuambia Floyd hayo na amenihakikishia bado nipo kwenye orodha yake,"amesema.
Khan anapanda ulingoni usiku wa kesho ukumbi wa MGM Grand Garden Arena mjini Las Vegas, Marekani kuzipiga na Luis Collazo, hilo likiwa pambano la utangulizi kablaya Mayweather kuzipiga na Marcos Maidana.
Mayweather tayari kwa pambano na Marcos Maidana kesho
0 comments:
Post a Comment