MWANASOKA wa kimataifa wa Kenya, Victor Wanyama anataka kumfuata kocha Mauricio Pochettino aliyetoka Southampton na kutua Tottenham.
Kiungo huyo Mkenya aliweka wazi wiki hii kwamba Saints walifanya kosa kumruhusu mwalimu huyo Muragentina kuondoka, walitakiwa kumbakiza.
Wanyama amenufaika chini ya Pochettino akicheza nafasi ya kiungo mkabaji na kuisaidia Southampton kupunguza idadi ya mabao ya kufungwa.
Atamfuata kocha wake Spurs? Victor Wanyama (kusgoto) anaweza kumfuata kocha wake wa zamani, Mauricio Pochettino aliyehamia Tottenham
Alitua klabu hiyo kwa dau la Pauni Milioni 12 msimu uliopita na chini ya Pochettino akawa tegemeo la timu hiyo.
Tottenham ina wasiwasi wa kumpoteza mchezaji aneyetakiwa na Chelsea, Paulinho- pamoja na Sandro na Etienne Capoue ambao wote wanatakiwa na Napoli.
Wanyama amesema: "Nimejifunza mengi kutoka kwake, amenifunza mengi kuliko ndiyo maana nimekuwa mchezaji mzuri na kuna tofauti kubwa sana ukilinganisha na nilivyokuwa Celtic. Amechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo yangu," .
0 comments:
Post a Comment