// Disable text selection (not fully reliable)
function disableSelection(element) {
element.setAttribute('unselectable', 'on');
element.style.userSelect = 'none';
element.style.MozUserSelect = 'none';
element.style.webkitUserSelect = 'none';
}
// Apply to the entire document body
document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() {
disableSelection(document.body);
});
MBEYA CITY YAANZA VYEMA MICHUANO MIPYA CECAFA, WAPIGA MTU TATU, WAUWAJI MWAGANE YEYA, PUAL NONGA NA MTU MPYA THEMI FELIX KUTOKA KAGERA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINEMBEYA CITY YAANZA VYEMA MICHUANO MIPYA CECAFA, WAPIGA MTU TATU, WAUWAJI MWAGANE YEYA, PUAL NONGA NA MTU MPYA THEMI FELIX KUTOKA KAGERA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
MBEYA CITY YAANZA VYEMA MICHUANO MIPYA CECAFA, WAPIGA MTU TATU, WAUWAJI MWAGANE YEYA, PUAL NONGA NA MTU MPYA THEMI FELIX KUTOKA KAGERA
Na Rodgers Mulindwa, KHARTOUM WAWAKILISHI wa Tanzania Bara katika michuano mipya ya klabu ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) iitwayo Nile Basin, Mbeya City wameanza vizuri leo baada ya kuifunga mabao 3-2 Academie Tchite ya Burundi mjini Khartoum, Sudan. Mabao ya Mbeya City katika mchezo huo wa Kundi B yamefungwa na Paul Nonga dakika ya 15, mshambuliaji mpya Themi Felix kutoka Kagera Sugar dakika ya 27 na Mwagane Yeya dakika ya 37. Mabao ya timu ya Burundi yamefungwa na Rashid Patient dakika ya 10 na Munirakiza Cedric dakika ya 68.
Wachezaji wa Mbeya City wakishangilia moja ya mabao yao leo
Ushindi huo unawaweka Mbeya City katika nafasi nzuri ya kutinga Robo Fainali ya michuano hiyo. Mapema katika mechi za ufunguzi jana, mabao saba yalitinga nyavuni, Victoria University ya Uganda ikiilaza 1-0 Malakia ya Sudan Kusini, El-Merreikh waliichapa 3-0 Polisi ya Zanzibar na El-Shandi waliilaza 2-1 Dkhill ya Djibouti. Michuano hiyo inashirikisha mabingwa wa Kombe la FA na washindi wa pili wa Ligi Kuu wa nchi wanachama wa CECAFA. Mbeya City imechukua nafasi ya Azam FC, washindi wa pili wa Ligi Kuu msimu uliopita, ambao wamejitoa. Simba SC ambao wangechukua nafasi ya Azam, wakati taarifa inakuja ya kufanyika kwa mara ya kwanza michuano hiyo, walikuwa wamekwishavunja kambi na wachezaji wao wote walikuwa wameruhusiwa likizo.
Paul Nonga wa Mbeya City akipambana na Kabeya Kalala wa Academie Tchite aliyelala kuondosha mpira kwenye hatari
Deogratius Julius wa Mbeya City akipambana na Dieudonne Issa wa Academie Tchite
Mwagane Yeya wa Mbeya City akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Academie Tchite
Item Reviewed: MBEYA CITY YAANZA VYEMA MICHUANO MIPYA CECAFA, WAPIGA MTU TATU, WAUWAJI MWAGANE YEYA, PUAL NONGA NA MTU MPYA THEMI FELIX KUTOKA KAGERA
Rating: 5
Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
Lookman crowned African footballer of the year
-
The 2024 Confederation of African Football (CAF) Award took center stage on
Monday night, with the best talents in African football emerging winners.
The...
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment