// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAZEMBE YAWARUHUSU SAMATTA, ULIMWENGU KWENDA KUIONGEZEA NGUVU STARS ZIMBABWE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAZEMBE YAWARUHUSU SAMATTA, ULIMWENGU KWENDA KUIONGEZEA NGUVU STARS ZIMBABWE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, May 29, 2014

    MAZEMBE YAWARUHUSU SAMATTA, ULIMWENGU KWENDA KUIONGEZEA NGUVU STARS ZIMBABWE

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    HATIMAYE klabu ya TP Mazembe imewaruhusu wachezaji wake Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kujiunga na timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo tayari imewasili Harare, Zimbabwe kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika.
    Taifa Stars itacheza na Zimbabwe ‘Mighty Warriors’ katika mechi ya marudiano raundi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.  Mechi hiyo itachezwa Jumapili (Juni 1 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa jijini Harare.
    Mbwana Samatta atakwenda Zimbabwe kuiongezea nguvu Taifa Stars

    Samatta na Ulimwengu watawasili Harare kesho Saa 3.40 usiku kwa ndege ya Kenya Airways na watajiunga na TP Mazembe mara baada ya mchezo huo ambapo Juni 2 mwaka huu, wakienda moja kwa moja Ndola, Zambia ambapo timu yao imepiga kambi kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zamalek Juni 7.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAZEMBE YAWARUHUSU SAMATTA, ULIMWENGU KWENDA KUIONGEZEA NGUVU STARS ZIMBABWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top